1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Ukraine yasema inaendelea kusonga mbele ndani ya Urusi

14 Agosti 2024

Ukraine imesema jana kuwa hivi sasa inadhibiti maeneo 74 ya makaazi katika mkoa wa Kursk nchini Urusi, na ilikuwa inaendelea kusonga mbele, kwa umbali wa kati ya kilomita moja hadi tatu katika muda wa saa 24.

https://p.dw.com/p/4jQvj
Urusi | Askari wa Ukreni wakiwa wamesimama karibu na jengo mjini Sudzha, mkoa wa Kursk
Askari wa Ukreni wakiwa wamesimama karibu na jengo mjini Sudzha, mkoa wa Kursk, baada ya operesheni ya kustukiza ya uvamizi ndani ya Urusi.Picha: Youtube

Ukraine imesema jana kuwa hivi sasa inadhibiti maeneo 74 ya makaazi katika mkoa wa Kursk nchini Urusi, na ilikuwa inaendelea kusonga mbele, kwa umbali wa kati ya kilomita moja hadi tatu katika muda wa saa 24.

Maelezo hayo ya Kyiv yanakinzana na taswira inayochorwa na Urusi, ambako Meja Jenerali Apti Alaudinov alisema vikosi vya Ukraine vimedhibitiwa, huku wizara ya ulinzi ikisema mashambulizi yametibuliwa katika vijiji umbali wa kilomita 26 hadi 28 kutoka mpakani.

Mkoa wa Kursk wa Urusi | Safu ya malori ya jeshi la Urusi yalioharibiwa na vikosi vya Ukraine
Safu ya malori ya jeshi la Urusi yalioharibiwa na vikosi vya Ukraine baada ya uvamizi Kursk.Picha: Anatoliy Zhdanov/dpa/Kommersant Publishing House/AP/picture alliance

Soma pia: Putin asema Ukraine itapokea jibu stahiki kuhusu uvamizi wake Kursk

Ukraine iliifanyia Urusi shambulio ka kustukiza kwa kumuaga maelfu ya wanajeshi katika mkoa wa magharibi wa Kursk wiki iliyopita, katika operesheni ambayo imeipta Ukraine mafanikio yake makubwa zaidi ya uwanja wa vita tangu mwaka 2022, baada ya miezi kadhaa ya kuzidiwa mbinu na Urusi.