1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine yakabiliwa na mapigano makali

4 Agosti 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kuwa vikosi vya nchi yake vimekabiliwa na mapigano makali katika sehemu zote za mapambano lakini hata hivyo bado wanashinda.

https://p.dw.com/p/4UlgF
Litauen Vilnius | NATO-Gipfeltreffen 2023 | Selenskyj spricht zur Presse
Picha: Ints Kalnins/REUTERS

Zelensky alitoa matamshi hayo jana akisema kuwa mapigano ni makali kila mahali na kwamba vikosi vyake vinapambana kwenye maeneo ya mashariki ya Kupiansk, Lyman, Bakhmut, Mariinka na Avdiivka sambamba na upande wa kusini.

Soma pia: Urusi yaituhumu Ukraine kwa mashambulizi mjini Moscow

Ukraine ilianzisha mashambulizi yake yaliyokuwa yakisubiriwa kwa muda mrefu mnamo mwezi Juni ili kuvirudisha nyuma vikosi vya Urusi kutoka maeneo ya mashariki na kusini lakini tangu wakati huo imepata mafanikio kidogo.

Soma pia: Urusi yafanya mazoezi ya kijeshi katika Bahari Nyeusi

Mwishoni mwa msimu wa majira ya joto uliopita, Ukraine ilifanikiwa kuyachukua tena baadhi ya maeneo karibu na mji wa Kherson na Kharkiv katika mashambulizi yake.