1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine: Tumevirejesha nyuma vikosi vya Urusi huko Bakhmut

16 Mei 2023

Naibu waziri wa ulinzi wa Ukraine amesema kwamba wanajeshi wa Kyiv wamevirejesha nyuma vikosi vya Urusi kunako maeneo kadhaa karibu na mji wa mashariki mwa nchi hiyo unaokabiliwa na mapigano makali wa Bakhmut.

https://p.dw.com/p/4RSHx
Ukraine Krieg Panzer Donetsk Region
Picha: Vincenzo Circosta/AA/picture alliance

Katika taarifa iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii, Ganna Malyar amebaini kuwa katika siku chache zilizopita, wanajeshi wa Ukraine walikomboa karibu kilomita 20 za mraba kaskazini na kusini mwa viunga vya mji wa Bakhmut.

Hayo yanajiri wakati viongozi wa Mataifa 46 wa Baraza la Haki na Demokrasia barani Ulaya wamekutana nchini Iceland kuonyesha mshikamano dhidi ya Moscow huku mataifa kadhaa ya Ulaya yakiahidi kuongeza misaada ya kijeshi kwa Ukraine.