1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine imesema makamada wa jeshi wa Urusi wameuwawa Crimea

23 Septemba 2023

Mamlaka nchini Ukraine zimesema idadi kadhaa ya watu wakiwemo makamanda waandamizi wa jeshi la wanamaji la Urusi wameuawa au kujeruhiwa Crimea.

https://p.dw.com/p/4Wixf
Russland Rauch aus einem russischen Marinehauptquartier aufsteigt in Sewastopol
Picha: Planet Labs PBC/AFP

Mamlaka nchini Ukraine zimesema idadi kadhaa ya watu wakiwemo makamanda waandamizi wa jeshi la wanamaji la Urusi wameuawa au kujeruhiwa baada ya kufanyika shambulizi la kombora kwenye makao makuu ya jeshi la majini la Urusi yaliopo katika Bahari Nyeusi kwenye rasi ya Crimea.

Ukraine inasema shambulizi hilo kubwa la Ijumaa lilifanyika wakati uongozi wa jeshi la maji ukiwa mkutanoni.

Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa wa Ukraine, Kyrylo Budanov, amenukuliwa Sauti ya Amerika (VoA) akisema watu tisa wameuwawa, wakiwemo majenerali wa kijeshi.

Kwa upande wake, Urusi ilisema mmoja miongoni mwa wanajeshi wake hajulikani alipo baada ya shambulizi hilo. Serikali ya Ukraine  imeapa kulirudisha eneo la Crimea katika mamlaka yake baada ya kunyakuliwa na Urusi mwaka 2014.