1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza, Marekani zaishutumu Urusi kwa ujasusi mitandaoni

8 Desemba 2023

Serikali ya Uingereza na Marekani zimezishutumu idara za ujasusi za Urusi kwa kujihusisha na kampeni endelevu za ujasusi mtandaoni dhidi ya wanasiasa maarufu, waandishi wa habari na mashirika yasiyo ya kiserikali.

https://p.dw.com/p/4Zufl
Uingereza na Marekani zinadai Urusi inafanya ujasusi kwenye mitandao ya kijamii.
Uingereza na Marekani zinadai Urusi inafanya ujasusi kwenye mitandao ya kijamii.Picha: Panthermedia/IMAGO

Kwenye madai haya ya karibuni, Waziri wa Mambo ya Nje David Cameron amesema Idara ya Usalama ya Shirikisho la Urusi (FSB) ilihusika na "majaribio yaliyofeli ya kuingilia mchakato wa kisiasa wa Uingereza" na tayari imemuita balozi wa Urusi mjini London kuhusiana na suala hilo.

Lakini nchini Marekani, waendesha mashtaka wameyafuta mashtaka dhidi ya raia wawili wa Urusi waliodaiwa kudukua mitandao ya kompyuta nchini Uingereza, Marekani na nchi nyingine za jumuiya ya NATO.

Soma zaidi: Zelensky ameonya dhidi ya kusambaratika kwa ushirikiano wa mataifa ya Magharibi

Urusi imekuwa ikishukiwa kuingilia siasa za Uingereza huko nyuma, ikiwa ni pamoja na kura ya maoni iliyoleta mgawanyiko ya Brexit 2016, lakini serikali ya taifa hilo ya Conservative imekosolewa kwa kushindwa kuchunguza.