1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhispania yashinda Kombe la Dunia la Wanawake

20 Agosti 2023

Uhispania imeshinda Kombe la Dunia la Wanawake kwa mara ya kwanza katika historia yao. Bao pekee la nahodha Olga Carmona lilitosha kuwapa ushindi Uhispania wa 1 - 0 dhidi ya England katika mchezo wa fainali.

https://p.dw.com/p/4VNT6
FIFA Fußball Frauen-WM | Finale Spanien vs England
Picha: Frank Fife/AFP/Getty Images

Uhispania ilionyesha mchezo wa hali ya juu na kupata nafasi nyingi za kufunga ikiwa ni pamoja na penalti waliyopoteza katika kipindi cha pili.

Ushindi huo wa Uhispania ni ahueni kwa Jorge Vilda na shirikisho la soka la Uhispania, ambalo lilimuwamini kocha huyo hata baada ya wachezaji 15 mwaka jana kusema hawakutaka kuiwakilisha nchi yao chini yake. 

Kocha wa England Sarina Wiegman ambaye sasa amepoteza fainali mbili mfululizo, na mafanikio yake ya Ulaya hawawezi kuwa na malalamiko yoyote.