1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiAfrika

Uganda kuzungumza na Tanzania ili kupitisha mafuta yake

15 Februari 2024

Waziri wa nishati wa Uganda Ruth Nankabirwa amesema nchi hiyo inafanya mazungumzo na Tanzania ili kusafirisha bidhaa zake zote za mafuta kupitia Dar es Salaam. Hii ikimaanisha hawataitumia bandari ya Mombasa, Kenya.

https://p.dw.com/p/4cRtG
Rais wa Uganda | Yoweri Musevini
Rais wa Uganda Yoweri MuseveniPicha: ABUBAKER LUBOWA/REUTERS

Uganda haijaridhishwa na mfumo wa muda mrefu ambao kampuni za mafuta za Uganda hununua asilimia 90 ya bidhaa zao kupitia kampuni tanzu za nchini Kenya.

Rais Yoweri Museveni amekuwa akilalamika kuwa hiyo inaiweka nchi yake katika usumbufu wa soko la mafuta na bei za juu za mafuta. Katika kujibu, Uganda ilitangaza kuwa itakabidhi haki za kipekee za usambazaji wa bidhaa zote za mafuta kwa kitengo cha kampuni ya kimataifa ya nishati Vitol.

soma pia:Bomba la mafuta la Afrika Mashariki lakabiliwa na mtikisiko

Uganda ilipanga bidhaa zote ziwasili kupitia Kenya, lakini Waziri Nankabirwa amesema serikali ya Kenya ilikataa kutoa leseni inayohitajika.

Na sasa kamati za kiufundi za Uganda na Tanzania zinafanya mazungumzo. Amesema hivi karibuni atakutana na Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania kujadili suala hilo.