1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uganda yakumbwa na mripuko wa pili katika siku mbili

26 Oktoba 2021

Mtu mmoja amekufa na kadhaa kujeruhiwa katika mripuko Jumatatu kwenye basi karibu na mji mkuu wa Uganda, Kampala huku Rais Yoweri Museveni akidokeza kuwa ulisababishwa na bomu.

https://p.dw.com/p/42B28
Explosion Bus Uganda
Picha: Joseph Kiggundu/Xinhua/picture alliance

Mripuko mwingine mjini humo Jumamosi ulimuuwa mtu mmoja na kuwajeruhi wengine watatu, ambao polisi illisema ni "kitendo cha ugaidi wa ndani" na ambao kundi linalojiita Dola la Kiislamu - IS lilidai kuhusika.

Msemaji wa polisi ya Uganda Fred Enanga amesema watalaamu wa mabomu walipelekwa katika eneo la Lungala baada ya mripuko mkali wa jana kwenye basi la kampuni ya Swift Safaris mwendo wa saa kumi na moja jioni.

Enanga hakutoa maelezo zaidi kuhusu kinachoshukiwa kusababisha mripuko huo.

Lungala ni karibu kilomita 35 magharibi mwa Kampala, kwenye mojawapo ya barabara zenye shughuli nyingi zaidi inayounganisha Uganda na Tanzania, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo