Ufisadi Kenya: Mihimili mitatu ya serikali yapewa siku 30
22 Januari 2024Kwenye mkutano wa faragha katika ikulu ya Nairobi kati ya Rais William Ruto, Jaji Mkuu Martha Koome, na Spika wa Bunge Moses Wetangula, ilikubaliwa kuwa mihimili hiyo mitatu ingeliwasilisha mapendekezo hayo kwa Baraza la Taifa la Kutekeleza Haki kwa lengo la kumaliza mvutano kati ya serikali ya Ruto na Mahakama kuhusu madai ya rushwa dhidi ya majaji kwa manufaa ya wananchi.
Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, viongozi kwenye mihimili hiyo mitatu ya serikali waliafikiana kuunda sera, miongozo na kanuni na miswada ili kuyafanikisha malengo yao.
Mkutano huo wa siku ya Jumatatu (Januari 22) huenda ukapunguza misuguano kati ya baraza la mawaziri chini ya Rais Ruto na Idara ya Mahakama ambayo imekuwa ikishuhudiwa katika kipindi kirefu cha mwaka huu.