1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa yataka lipelekwe haraka Kikosi cha UM huko Ivory Coast

17 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFiO
NEW YORK: Waziri wa Mambo ya Ulinzi wa Ufaransa Bibi Michèle Alliot-Marie ametoa mwito wa kupelekwa haraka Kikosi cha UM cha kuhifadhi amani nchini Ivory Coast. Kwa sababu hiyo Ufaransa imelipa Baraza la Usalama la UM mswada wa azimio kuhusu kikosi hicho, alisema Waziri huyo baada ya kukutana mjini New York na Katibu Mkuu wa UM Kofi Annan. Lazima juhudi za amani zisisitizwe kwa kuchukuliwa hatua za kuyapokonya silaha makundi yanayohasimiana katika nchi hiyo yenye vita vya ndani, alisema Bibi Alliot-Marie. Kwa sababu hiyo ni muhimu sana kipelekwe kikosi cha amani cha UM, alisisitiza. Nayo Marekani imesema ina shaka zake kuhusu kiwango kikubwa cha wanajeshi 6,200 wa UM nchini Ivory Coast.