1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa yaongeza upekuzi mipakani kudhibiti uhamiaji

Josephat Charo
2 Oktoba 2024

Ufaransa inapania kurefusha upekuzi katika mipaka yake kudhibiti uhamiaji usio halali kwa muda mrefu kadri itakavyohitajika.

https://p.dw.com/p/4lKEF
Ufaransa | Michel Barnier
Waziri Mkuu wa Ufaransa, Michel Barnier.Picha: Alain Jocard/AFP/Getty Images

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu wa Ufaransa Michel Barnier wakati alipozindua mpango mpya wa utawala wake bungeni jana Jumanne.

Barnier alisema udhibiti wa mpakani unaotarajiwa kufika mwisho mwezi huu wa Oktoba utarefushwa, akiangazia hatua kama hizo zilizochukuliwa nchini Ujerumani mwezi uliopita.

Soma zaidi: Ufaransa yaahidi kuimarisha uhusiano na Uingereza

Barnier pia aliahidi kuimarisha utendaji kwa ajili ya wakala wa ulinzi wa mipaka wa Ulaya, Frontex, ili kuboresha udhibiti na usimamizi wa mipaka ya nje ya Umoja wa Ulaya.