1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa yajadili kuwaondoa wanajeshi wake Niger

Josephat Charo
6 Septemba 2023

Ufaransa inafanya mazungumzo na watala wa kijeshi nchini Niger kuhusu kuwaondoa baadhi ya wanajeshi wake wanauhudumu nchini humo kama sehemu ya vita dhidi ya wapiganaji wa jihadi eneo la Sahel.

https://p.dw.com/p/4Vzcc
Niger Niamey | französische Luftwaffenbasis
Picha: ALAIN JOCARD/AFP/Getty Images

Jeshi la Ufaransa linafanya mazungumzo na utawala wa kijeshi wa Niger kuhusu kuwaondoa baadhi ya wanajeshi wake nchini humo kufuatia mapinduzi ya kijeshi.

Chanzo kimoja katika wizara ya ulinzi ya Ufaransa kimeliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba mazungumzo kuhusu kuondoka kwa baadhi ya wanajeshi yameanza lakini hakikutoa taarifa zaidi.

Chanzo hicho pia kimedokeza kwamba vikosi vya Ufaransa vimesimamishwa visitekeleze majukumu yake Niger tangu operesheni dhidi ya ugaidi zilipositishwa kufuatia mapinduzi ya kijeshi.

Kiasi wanajeshi 1,500 wako nchini Niger kama sehemu ya vita vipana vya Ufaransa dhidi ya makundi ya wapiganaji wa jihad katika eneo la Sahel. Niger iligeuka kuwa eneo muhimu kwa Ufaransa baada ya mapinduzi ya kijeshi kuwalazimu wanajeshi wa Ufaransa kuondoka kutoka nchi jirani za Mali na Burkina Faso.