1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa yachukua hatua kali kupambana na machafuko

8 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEKL

Paris:

Serikali ya Ufaransa leo imetekeleza sheria ya zamani ya miaka 50 iliyopita iliyotumiwa mwanzoni mwa vita vya Algeria. Sheria hiyo inawaruhusu Maafisa kutangaza amri ya kutotembea usiku katika yale maeneo yaliyokumbwa na siku 12 za machafuko nchini humo. Baraza la Mawaziri, kwa mujibu wa sheria nambari 55 kifungu cha 385 ya Aprili 3, 1955, linaweza kutangaza sheria ya hatari kwa baadhi ya maeneo maalumu na Viongozi wa serikali za mitaa wanaweza kutangaza amri kuhusu nyendo za watu na magari kwa muda maalumu. Sheria hiyo imetumiwa mara moja wakati wa vita vya Algeria vya mwaka 1954 mpaka 1962. Serikali ya Rais Francois Mitterrand imeitumia sheria hiyo mwaka 1984 kwa lengo la kuleta utulivu na amani katika New Caledonia. Serikali ya Ufaransa imelazimika kutumia sheria hiyo kutokana na machafuko ya Vijana yanayoendelea nchini humo.