1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa kuisaidia Niger

30 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEpX

Paris:

Rais Jacque Chirac wa Ufaransa ametangaza leo kuwa nchi yake itaongeza mara tatu misaada yake ya chakula kwa Niger iliyokumbwa na balaa la njaa. Ufaransa itatoa Dollar millioni 5.57 mwaka huu ili kusaidia kuokoa maisha ya Watoto elfu kadhaa wanaotapia mlo. Rais Chirac amesema kuwa Ufaransa itaongeza pia maradufu michango yake ya fedha kwenye Mpango wa Chakula Ulimwenguni. Euro Millioni moja zitatumiwa kwa kuwapa chakula Wanafunzi katika zile sehemu zilizoathirika sana. Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ufaransa, Philippe Douste-Blazy, amewasili Niger leo kusimamia ugawaji wa misaada na kuamua kile kinachotakiwa zaidi. Umaskini na njaa husababisha kila mtoto mmoja kati ya wanne, wenye umri usiozidi miaka mitano, kufariki nchini Niger. Ukame na nzige vimeharibu mazao yote nchini humo.