1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UFARANSA IMEIONESHA UJERUMANI JINSI ITAVYOTETEA TAJI LAKE LA ULAYA

17 Novemba 2003

-KINYAN'GANYIRO CHA MATAIFA YA AFRIKA KUANIA TIKITI ZA KOMB E LA DUNIA 2006 UJERUMANI BRAZIL YAMUDU SULUHU BAO 1-1 NA PERU NA WANARIADHA WA ETHIOPIA WATIA FORA URENO NA JAPAN

https://p.dw.com/p/CHan

Mabingwa wa ulaya Ufaransa ambao walipigwa kumbo na Senegal katika duru ya kwanza ya Kombe la dunia mwaka jana huko Japan na Korea, wamerudi kutamba . Ujerumani ilizabwa mabao 3-0 na Ufaransa na baadae ikadai hayo yalikua maandalio makubwa na bora kabisa kwa mabingwa wa Ulaya.Kocha wa Ufaransa Jacques Santini amesema kwamba timu ya Ufaransa imeonesha ina jibu barabara kwa changamoto kutoka timu kali kama ile ya Ujerumani.Ufaransa sasa imerekodi ushindi wake wa 13 mfululizo-ushindi 1 zaidi kuliko rekodi yake ya hapo kabla iliowekwa 1984 enzi za Michel Platini-nahodha wao. Mchezo maridadi wa Zinedine Zidane ulikua chanzo cha ushindi wa Ufaransa dhidi ya Ujerumani.Lakini shukurani pia ziende kwa washambulizi wengine 2 Thierry Henry alietia bao 1 na David Trezeguet alietia mabao 2 kwa kuchezeshwa na Henry na Zidane.

Tangu ushindi wake dhidi ya England-Uingereza hapo Oktoba 2000,Ujerumani chini ya kocha wake Rudi Voeller imekuwa ikishindwa kufua dafu mbele ya timu kali .Ilishindwa na Argentina,Brazil,Uingereza,Ugfaransa,Itali,Holland na hata Spain. Dhidi ya mabingwa wa Ulaya-Ufaransa, Ujerumani ilitoa changamoto kali katika kipindi cha kwanza,lakini vishjindo vyao hivyo vilibainika katika kipindi cha pili ni kama vya darini vilivyoishia sakafuni.Huu ulikua mpambano wa mwisho wa timu ya Ujerumani mwaka huu.

Mabingwa wa dunia-Brazil walimudu nao suluhu tu ya bao 1:1 na Peru mjini Lima katika kanda ya Amerika Kusini ya kuania kufuzu kwa Kombe la dunia 2006 hapa Ujerumani.Bao la Peru limetiwa na Solano na hivyo kusawazisha bao la Brazil alilotia Rivaldo anaeichezea AC Milan ya Itali.

Katika kanda ya Afrika chipukizi wanaoinukia benin wamepiga hatua katika duru hii ya kwanza ya kuania tikiti za Kombe la dunia hapa Ujerumani.jana,benin iliitoa Madagascar kwa mabao 3-2 nyumbani Cotonou.Benin itakayocheza katika finali za Kombe la afrika la mataifa kwa mara ya kwanza mwakani nchini Tunisia,inasonga mbele kwa jumla ya ushindi wa mabao 4-3 kufuatia duru ya nyumbani na ugenini. Uganda ni timu nyengine iliovuka salama duru hii mwishoni mwa wiki licha ya kuzabwa mabao 3-1 na Mauritius.lakini bao la dakika ya mwisho la kitanzi-goldfen goal alilotia David Obua mnamo dakika ya 112 ya mchezo liliipatia Uganda ushindi jumla wa mabao 4-3.

Msumbiji imemtimua kocha wake Muukraine Viktor Bondarenko kufuatiwa kupigwa kumbo tangu nje ya Kombe la Afrika la Mataifa hata ya Kombe la dunia 2006. Pigo la jana ililopata Msumbiji kutoka Guinea limeitoa kutoka mashindano yote ya kimataifa tena kwa kipindi cha miaka 3 ijayo. Miongoni mwa timu nyengine zilizosonga mbele katika safari yao ya kuja Ujerumani 2006 kwa Kombe la dunia ni Algeria,Botswana,Gabon,Malawi,Mali,Rwanda,Sudan,Zambia ,Zimbabwe na Kenya.Kenya iliitimua Tanzania kwa mabao 3-0 .

Finali ya Kombe la klabu bingwa barani afrika kati ya Enyimba ya Nigeria na Ismailia ya Misri itachezwa duru ya kwanza mjini Aba,Nigeria Novemba 19 huku duru ya pili na ya mwisho ya kuamua bingwa itakua desemba 12 mjini Ismailia,Misri. Ismailia iliizaba Esperence mabao 3-1 katika duru ya pili ya nusu-finali ya Kombe hilo la klabu bingwa na hivyo imekata tiketi yake na Enyimba. Mabingwa wa afrika-Kamerun wanacheza mpambano wa kirafiki na Japan keshokutwa jumatano mjini Tokyo.

RUGBY:Finali ya kombe la dunia la rugby itachezwa jumamosi ijayo kati ya wenyeji Australia na Uingereza.Austrralia iliitoa New Zelanad wakati uingereza iliipiga kumbo jana Ufaransa.Ni rifu kutoka Afrika Kusini Andre Watson atakaechezesha kwa mara ya pili finali ya kombe la dunia.

RIADHA:Muethiopia Elfenesh Alemu amemtimua bingwa wa olimpik wa marathon Mjapan Naoko Takahashi na kushinda jana mbio za marathon za Tokyo.Hilo ni pigo la kwanza kwa bingwa huyo wa olimpik tangu 1998. Waethiopia wametia pia fora katika mashindano ya riadha ya mbio za nyika yalioandaliwa na shirikisho la riadha ulimwenguni-IAAF. Nchini Ureno. Katika masafa ya mita 10.000 Kenenisa Bekele alishinda kwa muda wa dakika 27 na sek.22 akifuatwa nafasi ya pili na Moses Kige kutoka Kenya.John Korir wa Kenya alikuja 3. Katika changamoto ya mita 5000 wanawake,Merima Damiao wa Ethiopia alishinda kwa muda wa dakika 16.22 akifuatwa nafasi ya pili na Mkenya Leah Malot.Isabella Ochichi alikuja nafasi ya 3.