1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiAfrika

Guinea yayumba kiuchumi baada ya bohari ya mafuta kuteketea

29 Desemba 2023

Taifa la Guinea linakabiliwa na matatizo makubwa ya kiuchumi na kijamii, takriban wiki mbili baada ya kutokea moto mkubwa katika bohari pekee la mafuta lililosababisha vifo vya watu 24 na uharibifu mkubwa wa mali.

https://p.dw.com/p/4ah97
Guinea | Bohari pekee ya mafuta Guinea ikiteketea kwa moto.
Moto uliozuka katika bohari pekee ya mafuta nchini GuineaPicha: AP Photo/picture alliance

Moto huo uliozuka Desemba 18 ulidhibitiwa baada ya siku 9. Hasira ya umma imeongezeka kutokana na uchumi kudorora, kupanda kwa mfumuko wa bei, mgao wa petroli na lori zikishindwa kusafirisha bidhaa muhimu.

Maduka mengi yamefungwa katika soko kuu la Conakry- Madina, huku shughuli zikiwa zimesitishwa pia kwenye bandari ya mji huo.

Soma pia:Idadi ya waliokufa kutokana na moto Guinea yafikia 23

Uhaba na mgao wa mafuta wa mafuta vimepelekea shughuli za kibiashara na kijamii kutatizika. Taifa hilo la Afrika Magharibi limesalia kuwa miongoni mwa nchi zenye maendeleo duni zaidi ulimwengunilicha ya kuwa na utajiri mkubwa wa madini yakiwemo dhahabu na bauxite.