1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaArmenia

Uchaguzi wa rais mpya wafanyika Nagorno Karabakh

9 Septemba 2023

Uchaguzi unafanyika leo katika mkoa wenye idadi kubwa ya Waarmenia wa Nagorno-Karabakh nchini Azerbaijan, kumchagua rais mpya huku mvutano kuhusu eneo hilo ukiongezeka kati ya mahasimu wakuu Azerbaijan na Armenia

https://p.dw.com/p/4W8mV
Maandamano katika mkoa wa Nagorno Karabakh kupinga kufungwa kwa barabara ya Lachin mnamo Julai 25,2023
Maandamano katika mkoa wa Nagorno KarabakhPicha: Alexander Patrin/TASS/dpa/picture alliance

Azerbaijan imeutaja uchaguzi huo kuwa hatua nyingine ya uchokozi mkubwa na ukiukaji wa wazi wa uhuru wake na uadilifu wa eneo hilo. Mkuu wa baraza la usalama la serikali hiyo ya uasi Samvel Shahramanyan, anaonekana kuwa na uwezekano mkubwa wa kumrithi Arayik Harutyunyan aliyejiuzulu mnamo Septemba mosi.

Armenia na Azerbaijan zimekuwa zikishtumiana kwa mashambulizi ya kuvuka mpaka

Katika miezi ya hivi karibuni, Armenia na Azerbaijan zimekuwa zikishtumiana kwa mashambulizi ya kuvuka mpaka.Armenia imeonya kuhusu hatari ya mzozo mpya, ikisema Azerbaijan imekuwa ikikusanya wanajeshi kwenye mpaka wa pamoja wa nchi hizo na karibu na Nagorno-Karabakh. Siku ya Ijumaa, wizara ya mambo ya nje ya Azerbaijan iliishutumu Armenia kwa kukiuka makubaliano ya awali na kuanza kufanya uchokozi wa namna mbalimbali ukiwemo wa kisiasa na wa kijeshi.