1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tuzo ya Ujerumani na Afrika yaenda Tanzania na Madagascar

Sekione Kitojo
28 Novemba 2018

Tuzo ya Ujerumani na Afrika mwaka huu imewaendea wanaharakati wawili kutoka barani Afrika. Gerald Bigurube kutoka Tanzania na Clovis  Razafimalala kutoka Madagascar wamepata kwa pamoja tuzo hiyo inayotolewa kila mwaka.

https://p.dw.com/p/392iT
Deutschland Deutscher Afrikapreis 2018 in Berlin u.a. mit Wolfgang Schäuble
Picha: Deutsche Afrika-Stiftung

Kwa nini  mara  hii  lakini  tuzo  hiyo imetolewa  kwa  wanaharakati  wa  ulinzi  wa  mazingira. Mkuu  wa  jopo la  majaji  kwa  ajili  ya  tuzo  hiyo Volker Faigle  ameweka  wazi  wakati wa  hotuba  yake, kwamba  mwanamfalme  wa  Uingereza  wiki  chache zilizopita  alipokuwa  akifungua  mkutano wa  kimataifa  alitoa  wito  wa kuzuwia  matumizi  ya  kupindukia  ya  ardhi  ili  kuzuwia athari za mabadiliko  ya  tabia  nchi. 

Deutschland Deutscher Afrikapreis 2018 in Berlin u.a. mit Wolfgang Schäuble
Wanaharakati wawili Gerald Bigurube wa Tanzania (kushoto) na Clovis Razafimalala wa Madagascar (kulia) wakiwa pamoja na jopo la majaji pamoja na viongozi wa serikali ya UjerumaniPicha: Deutsche Afrika-Stiftung

Ni  wito  muhimu  kama  anavyoeleza  rais  wa  majaji  Volker  Faigle waliowachagua wanaharakati  hao  wawili  wa   kulinda  mazingira kutoka  Afrika.

"Jioni  ya  leo sisi  ni  mashahidi , wa  watu  hawa  ambao  wameweza kujitolea  na  kupambana   na  hali  hii  kutoka  katika  bara  ambalo  ni jirani  yetu  la  Afrika. Watu  ambao  wanataka kuwalinda  watoto  wao pamoja  na  watoto  wetu  na  nchi zao. Pamoja  na  kuilinda  sayari yetu  na  kuonesha  hatari  inayokabili  uasili  pamoja  na  wanyamapori. Na  wanajihusisha  pamoja  na  kupambana  ili  kupata  sheria  ya  ulinzi kwa  hayo  yote."

Kuanzia  mwaka  1993  wakfu  wa  Ujerumani  na  Afrika  umejionesha kuwa  unapigania  amani , demokrasia  na  maendeleo  endelevu. Rais wa  bunge  la  Ujerumani  Wolfgang Schaueble ameeleza  kuhusu umuhimu  wa  bara  la  Afrika  kwa  Ulaya. Amesema  hali  ya  baadaye ya  bara  la  Ulaya  itaamuliwa  kupitia  ushirikiano  wa  pamoja  wa maendeleo  zaidi ya  bara  la  Afrika.

Deutschland Deutscher Afrikapreis 2018 in Berlin u.a. mit Wolfgang Schäuble
Wolfgang Schaueble , sipka wa bunge la Ujerumani(kulia na mshindi wa tuzo ya Ujerumani na Afrika Gerald Bigurube (kushoto)Picha: Deutsche Afrika-Stiftung

Hali  bora  ya  Afrika

Afrika  inahitaji  haraka  hali  bora ya  kiuchumi , lakini  haiwezi  kufanya  hivyo  peke  yake. "Hii inahusika zaidi  na  usalama  wa  muda  mrefu  wa  msingi  wa  maisha  ya  watu katika  bara  hilo. Mapambano  kuhusu  ulinzi  wa  uhai  anuai  pamoja na  wanyama  na  mimea ni  muhimu , na  ulinzi  katika  mabadiliko  ya tabia  nchi  ni  jukumu  muhimu  kwa  dunia  nzima."

Schaeuble  amesema  pia  kwamba  wanaharakati  hao ambao wamepata  tuzo  hii , Gerald Bigurube  na  Clovis Razafimalala wanahatarisha  mambo  mengi  binafsi.

"Wanahatarisha  mambo  mengi  ya  binafsi.  Biashara  haramu inayoingiza  fedha  nyingi  ya  miti ya  liwa  nchini Madagascar , pamoja miradi mikubwa  ambayo  inataka  kuharibu  maeneo  ya  wanyama  na mimea  nchini  Tanzania."

Deutschland Deutscher Afrikapreis 2018 in Berlin u.a. mit Wolfgang Schäuble
Spika wa bunge la Ujerumani Wolfgang Schaueble akimkabidhi tuzo Clovis Razafimalala kutoka MadagascarPicha: Deutsche Afrika-Stiftung

Bigurube  mwenye  umri  wa  miaka  66 amekuwa  tangu  miaka  40 iliyopita  ni  mwanaharakati  wa  ulinzi  wa  mazingira  nchini  Tanzania, ambaye  amehusika  zaidi  katika  eneo  maarufu  duniani  la   mbuga ya  Serengeti. Kwanza  alikuwa  mkuu  wa  shirika  la  taifa  la  hifadhi ya  wanyamapori  la  TANAPA, na  hivi  sasa  ni  mkurugenzi  wa  jamii ya  maeneo  ya  zoo  mjini  Frankfurt.

Jaji  wa  tuzo  hiyo Faigle  anamsifu  kuwa  ni  mjenga  muhimu  wa daraja. Bigurube  anasimama  kwa  ajili  ya  ulinzi  endelevu  wa mazingira, ambayo  yanakwenda  kwa  pamoja  na  mahitaji  muhimu  ya jamii  na  maendeleo.

Mwandishi: Daniel  Pelz /ZR/ Sekione  Kitojo

Mhariri: Mohammed Khelef