1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TUNIS: Rais wa Ufaransa Jacques Chirac amewasili Tunis kwa ziara rasmi na

4 Desemba 2003
https://p.dw.com/p/CFvE

akazungumuza kwanza na rais ZINE EL ABIDINE BEN ALI. Waziri wa kigeni wa Marekani Colin Powell pia alikuwa na ziara Jumaane iliopita katika nchi hiyo ya Afrika Kaskazini. Rais Chirac atashiriki kesho kwenye mkutano wa viongozi wa dola za Ulaya Kusini na Afrika Kaskazini. Mkutano huo, miongoni mwa mada nyinginezo, utazungumzia mapigano dhidi ya ugaidi wa kimataifa, na uhamiaji wa kimagendo wa watu kutoka Afrika Kaskazini kuelekea Ulaya.