1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TIRANA Maofisa wa kuhesabu kura wagomea kazi

6 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEx6

Makarani wa uchaguzi wameigomea kazi yao ya kuhesabu kura katika vituo kadhaa vya kupigia kura nchini Albania. Hatua hiyo itayachelewesha matokeo ya mwisho ya uchaguzi uliofanyika nchini humo Jumapili iliyopita. Ofisa wa tume ya uchaguzi amedhihirisha kwamba wafanyakazi hao waliisusia kazi yao katika vituo 15, huku masunduku mengi ya kura yakiwa bado hayajafunguliwa.

Matokeo ya mwanzo yanaonyesha chama cha upinzani cha Democratic, kinachoongozwa na Sali Berisha kimeshinda viti 53 kati ya viti vyote 100. Chama chake waziri mkuu Fastos Nano, kimetoa madai ya wizi wa kura. Waangalizi wa kimataifa wamesema uchaguzi huo haukufikia kiwango cha kimataifa. Chaguzi tatu za awali nchini Albania zilikumbwa na machafuko na wizi wa kura.