1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TIMU YA TAIFA YA ZANZIBAR KUJA UJERUMANI MEI 8 KWA DIMBA

25 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CHZB

BUNDESLIGA:

Tukianza na Ligi mashuhuri barani Ulaya:Klabu 3 –Bayern Munich ya Ujerumani, Chelsea ya Uingereza na FC Barcelona ya Spain zaelekea zimeshatia taji la ubingwa mfukoni kufuatia ushindi wao mwishoni mwa wiki:

Bayern Munich iko pointi 3 tu kabla kutawazwa mabingw wapya wa Ujerumani na kuivua taji Werder Bremen.Hii inafuatia ushindi wao wa mabao 3:1 dhidi ya Bochum na kushindwa tena kwa Schalke kufua dafu.Schalke iliraruliwa kwa mabao 4-1 na Hertha Berlin hapo jumamosi. Maboa kutoka Claudia Pizzaro,Michael Ballack na Roy Makaay yalitosha kuipatia Munich pointi 3 nyengine na sasa inaongoza Bundesliga kwa point 65 kwa 56 za Schalke.Stuttgart iko nafasi ya tatu baada ya kutoka suluhu 0:0 na Wolfsburg.Berlin iko sasa nafasi ya 4 ikiwa na jumla ya pointo 53.

Katika Ligi ya Uingereza-Premier League:Chelsea nayo imepiga hatua nyengine kutia kapuni ubingwa wake wa kwanza tangu kupita miaka 50 kwa kuizaba Fulham mabao 3:1.Mabao ya Joe Cole,Frank Lampard na Eidur Gudjohnsen yaliondoa shaka-shaka zilizosalia kwa Chelsea kutwa ubingwa.

Ama katika La LIGA-Ligi ya Spain, FC Barcelona iliendeleza mwanya wake wa pointi 6 kileleni mbele ya mabingwa mara kadhaa Real Madrid.Hii inafuatia ushindi wao wa mabao 4-0 dhidi ya Malaga.

KOMBE LA KLABU BINGWA BARANI AFRIKA:

Mabingwa wa zamani wa kombe la klabu bingwa barani Afrika-ASEC ABIDJAN ya Ivory Coast,wamekata tiketi yao ya robo-finali ya Kombe hilo baada ya jana kuitoa Dolphin Fc ya Nigeria kwa mikwaju ya penalty.

ASEC mabingwa 1988,waliipiga kumbo Dolphin kwa mabao 5-3 ya mikwaju ya adhabu baada ya timu hizi 2 kusimama sare 2:2.

Ajax capetown ya Afrika kusini nayo imeingia robo finali kwa mara ya kwanza kwa kuitimua nje Fello Star Labe ya Guinea kwa mabao 2:0 hapo jana.Zamalek ya Misri iliwika nyumbani kwa mabao 2:0 mbele ya AS Aviacao.

Timu nyengine zilizoingia robo-finali mwishoni mwa wiki ni : Al Ahli ya Misri;Etoile du Sahel na Esperence za Tunisia pamoja na Raja casablanca ya Morocco.Pia mabingwa Enyimba ya nigeria, wamekata tiketi yao.mabingwa 6 wa zamani wameingia robo-finali na firimbi italia Juni 25-26 kuanza duru hiyo.

Zanzibar ambayo imepata uanachama wa CAF mapema mwaka huu,imepania kuwa pia mwanachama wa FIFA-shirikisho la dimba ulimwenguni.Kuipigia upatu na kufahamika kuwa Zanzibar ina timu yake yenyewe ya Taifa mbali na ile ya Tanzania-bara, mjerumani wa kituo cha TV cha PRO-7,Oliver Pocher amekuwa akiipigia upatu zanzibar na hasda katika vipindi vyake vya TV akivaa T-shirtya manjano yenye Nembo ‘ZANZIBAR’.

Alhamisi hii usiku,kituo cha TV cha PRO-7 cha ujerumani kitaonesha dimba kati ya Zanzibar na Tanzania-bara.Nje ya chaki cha uwanja ataonekana makamo-rais wa ZFA Bw.Farouk Karim.

Mei 14 timu ya zanzibar imepangwa kucheza dimba mjini Hannover na timu ya mchanganyiko ya kituo hicho cha TV cha PRO-SIEBEN.

Bw.Farouk Karim alikua mjini Cologne mwishoni mwa wiki pamoja na mwenyeji wake Oliver Pocher walipotembea makumbusho ya Spoti na Olimpik.

Katika mbio za magari za Imola huko Itali jana, Michael Schumacher wa Ujerumani,alimaliza wapili mbele ya kiongozi wa mbio hizi msimu huu-mspain Fernando Alonso anaendesha gari la renault.Mastadi hao 2 walipapurana vikali na mwishoe,schumacher akabid i kuridhika na nafasi ya pili baada ya kuanza nafasi ya 13.