1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Timu ya soka ya wanawake ya Turbine Potsdam ya Ujerumani yatawazwa mabingwa barani Ulaya.

21 Mei 2010

Klabu ya Turbine Potsdam ya Ujerumani jana mjini Madrid ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa kandanda kwa vilabu vya wanawake barani Ulaya, baada ya kuchapa Olympique Lyon mabao 7-6.

https://p.dw.com/p/NTiG
Mchezaji Jennifer Zietz wa Turbine Potsdam akipambana na Elodie Thomas wa Olympique Lyon kwenye fainali za wanawake za kuwania taji la mabingwa barani Ulaya.Picha: picture alliance / dpa

Ushindi huo unakuja mnamo wakati ambapo macho na masikio ya mashabiki wa kabumbu duniani, kesho yakielekezwa  huko huko  Uhispania, katika fainali ya ligi ya mabingwa kwa wanaume kati ya Bayern Munich ya Ujerumani na Inter Milan ya Italia.

Mashabiki nchini Ujerumani wakiungwa mkono na kocha wa Portsdam wanasema ushindi wa kinadada hao wa kijerumani ni zulia jekundu kwa Bayern hapo kesho kutoroka na kombe mjini Madrid.

 Kocha wa timu hiyo, Bernd Schröder alisema kuwa timu yake ilishindwa kuchomoza vilivyo kipindi cha kwanza  lakini dimba likawa lao katika kipindi cha pili.

"kipindi cha kwanza hatukucheza vizuri.hakukuwa na kandanda ,tunaweza kucheza barabara.katika kipindi cha pili ndipo ulipocheza hasa kandanda na ni dhahiri tulistahilöi kushinda."

Kufuatia ushindi huo kocha huyo wa kina dada wa Postdam amewaambia mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich kufuata nyayo zao kwa kuonesha umahiri katika kusakata soka hapo kesho katika uwanja wa Barnabeu huko Madrid  dhidi ya Inter Milan

Timu zote mbili za Inter na Bayern zinatarajiwa kuandikisha historia hapo kesho.

Kikosi cha Bayern Tayari kimeshawasili mjini Madrid na kimeeleza matarajio ya fainali ya kesho kuwa kama mchezo mwingine wowote.

Fainali hiyo inajiri wakati ambapo macho yote yameelekezwa kwa makocha wawili wa timu hizo  louis Vaan Gal aliye na azma ya kuingozea Bayern mataji, na uvumi uliopo wa Jose Mourinho wa Inter kuiacha timu hiyo baada ya fainali ya kesho na kujiunga na timu ya Real Madrid. Na hili limezidishwa baada ya Mourinho kunukuliwa na vyombo vya habari akitoa wito kwa mashabiki wa Real kuishabikia Inter hapo kesho.

Vyombo vya habari nchini Italia vimetaja kikosi cha Inter kuwashirikisha Javier Zanetti  akishirikiana na Wesley Sneijder  na Samuel Eto'o pamoja na Diego Milito.Pia huenda Mkenya Mcdonald Mariga akawa mwanasoka wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kuingia dimbani katika fainali ya Ulaya.

Ngome ya Inter italindwa na kipa Julio Cesar na Lucio pamoja na Walter Samuel,na Maicon na Christian Chivu.

Huku upande wa Van Gaal ukishiriki fainali ya kesho bila ya Mfaransa Frank Ribery  aliyepewa marufuku ya kutoshiriki michuano mitatu baada ya kupewa kadi nyekundu wakati Bayern ilipocheza na Olympique Lyon katika Mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya kuwania taji hilo la mabingwa barani Ulaya.

Kukataliwa kwa rufaa aliyokata Ribery dhidi ya marufuku hiyo ili kumuezesha kushiriki fainali ya kesho, huenda imewacha pengo kwa washindi hao wa Bundesliga baada ya Mchezaji mwenza katika timu hiyo Philip Lahm  kueleza kuwa ni pigo kubwa kumkosa Ribery lakini Bayern Munich inatarajiya kuonesha mchezo mzuri vivyohivyo.

Mturuki Hamit Altintop aliyechukua nafasi yake katika mkondo wa pili wa nusu fainali anatarajiwa tena kuchukua nafasi hiyo hapo kesho kwenye fainali.

Kando na mabadiliko hayo van Gaal huenda akatumia kikosi kilicho chuana na Bremen kilichowashirikisha kipa Hans Joerg Butt,Philip Lahm na Mark van Bommel ,Bastian Shweinsteiger,pamoja na Arjen Robben na Mcroatia Ivica Olic  aliye chini ya Messi wa Barcelona kwa wingi wa mabao katika taji hilo la mabingwa barani Ulaya kwa tofauti ya bao moja pekee.

Mwandishi Maryam Abdalla

Mhariri:Aboubakary Liongo