1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Timu nne zawinda tiketi za mwisho za robo fainali ya CL

15 Machi 2021

Hatua ya 16 ya mwisho katika Champions League inakamilika wiki hii wakati Bayern Munich na Manchester City wakiwa na njia rahisi ya kutinga robo fainali lakini miamba wawili wa Madrid, Real na Atletico wana mlima

https://p.dw.com/p/3qetA
UEFA Champions League | Atletico Madrid v Chelsea
Picha: Octav Ganea/Inquam Photos/REUTERS

Hatua ya 16 ya mwisho katika Champions League inakamilika wiki hii wakati Bayern Munich na Manchester City wakiwa na njia rahisi ya kutinga robo fainali lakini miamba wawili wa Madrid, Real na Atletico wana kazi ya kufanya katika mechi zao za mkondo wa pili.

Real Madrid wanawaalika Atalanta kesho Jumanne wakiwa kifua mbele 1 – 0 wakati Atletico wanaelekea London Jumatano kuyapindua matokeo ya 1 – 0 dhidi ya Chelsea kama wangetaka kuwa kwenye droo ya Ijumaa ya nane za mwisho na nusu fainali.

Man City wanarejea Budapest kucheza Jumanne mechi yao ya nyumbani wakiwa kifua mbele 2 – 0 dhidi ya Borussia Moenchengladbach wakati Jumatano Bayern wanatarajia kupenya dhidi ya Lazio wakiwa mbele 4 – 1.

Liverpool, Porto, Borussia Dortmund na Paris Saint-Germain walifuzu wiki iliyopita.

AFP, DPA, AP, Reuters