1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tel Aviv. Rice azitaka Israel na Palestina kujiweka mbali na ghasia

14 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEIb

.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice yuko nchini Israel akiwa katika kituo chake cha nne katika ziara yake ya mashariki ya kati.

Anatarajiwa kukutana na viongozi wa Israel na Palestina kwa mazungumzo yanayolenga katika kuzishawishi pande zote mbili kuanza tena juhudi za kufufua hatua za kuleta amani.

Katika hotuba aliyoitoa jioni waziri huyo wa mambo ya kigeni wa Marekani ameisifu hatua ya Israel ya kujiondoa kutoka Gaza lakini amesema kuwa pande zote mbili zinapaswa kuchukua hatua muhimu kujitenga na ghasia.

Rice amekwenda Israel akitokea Saudi Arabia jana Jumapili, ambako amefanya mazungumzo na waziri wa mambo ya kigeni Saud al-Faisal. Pia anatarajiwa kwenda nchini Jordan.