1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tehran. Katibu mkuu Kofi Annan akutana na maafisa wa Iran.

3 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDFg

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa amekutana na maafisa wa Iran wakati akitafuta kuungwa mkono kwa makubaliano ya kusitisha mapigano ambayo yamemaliza mzozo uliodumu kwa muda wa mwezi mmoja baina ya Israel na wanamgambo wa Hizbollah nchini Lebanon.

Jana Jumamosi, katibu mkuu Kofi Annan alikutana na waziri wa mambo ya kigeni Manouchehr Mottaki , ambaye amesema kuwa Iran inaungamkono moja kwa moja makubaliano yaliyosimamiwa na umoja wa mataifa ya kusitisha mapigano nchini Lebanon.

Iran inaaminika kwa kiwango kikubwa kuwa ni mfadhili mkubwa wa silaha wa kundi la Hizbollah , lakini nchi hiyo inasisitiza kuwa msaada wake ni wa kisiasa tu.

Annan pia alikuwa na mazungumzo na mjumbe wa majadiliano wa nchi hiyo katika mazungumzo ya kinuklia Ali Larijani, na kueleza kuwa mazungumzo yao yalikuwa ya mafanikio.

Hii inakuja siku mbili baada ya Iran kushindwa kufuata muda wa mwisho uliotolewa na umoja wa mataifa kusitisha shughuli zake za urutubishaji wa madini ya Urani. Mawaziri wa mambo ya kigeni wa mataifa ya umoja wa Ulaya wamekubaliana kuipa Iran wiki mbili zaidi kufafanua mzimamo wako.

Marekani imekuwa ikisisitiza kuiwekea vikwazo Iran, lakini mawaziri hao wa umoja wa Ulaya wanasema kuwa wanahitaji mazungumzo zaidi na Iran.