1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tedesco: Sina hofu na ukame wa mabao wa Lukaku

1 Julai 2024

Mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, hajafunga katika mashindano yanayoendelea ya Euro 2024.

https://p.dw.com/p/4hkAv
Euro 2024 | Spiel Belgien gegen Rumänien
Mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu LukakuPicha: Peter De Voecht/Photo News/IMAGO

Magoli kadhaa aliyoyafunga katika hatua ya makundi yalikataliwa kwasababu tofauti ikiwemo kuotea au kuunawa mpira.

Kocha wake Domenico Tedesco lakini anasema hana wasiwasi kuhusiana na ukame wake wa mabao kwani ana uhakika kwamba atakapokuwa makini zaidi langoni, basi bila shaka atautikisa wavu.

"Si mtu anayehisi shinikizo, anajiwekea shinikizo mwenyewe kwasababu anataka kufunga, anataka kuwa kiongozi na ndivyo alivyo. Ni mmoja wa wachezaji muhimu katika timu hii na kwetu ni muhimu afunge mabao lakini hatusemi ni mshambuliaji mzuri au la kutokana na ufungaji wake, anajinyima sana kwa ajili ya timu, anastahili kuwa mtulivu tu na mambo yatakuwa sawa," alisema Tedesco.

Vyanzo: Reuters/DPAE