1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tebogo wa Botswana nusra aibuke bingwa wa dunia

21 Agosti 2023

Mwanariadha wa Marekani Noah Lyles ndiye bingwa wa dunia kwa sasa baada ya kutimka kwa sekunde 9.83 hapo Jumapili katika mashindano ya dunia ya riadha yanayoendelea huko Budapest.

https://p.dw.com/p/4VPVY
Michezo Riadha - Mashindano ya dunia ya riadha 2023 I Fainali mita 100 wanaume I Letsile Tebogo
Letsile Tebogo wa Botswana akiwa na medali yake ya fedhaPicha: Song Yanhua/Xinhua News Agency/picture alliance

Letsile Tebogo wa Botswana aliinyakulia nchi yake na bara zima la Afrika medali ya fedha ambayo ndiyo medali ya kwanza ya Afrika katika mita 100 kwenye historia ya mashindano hayo.

Tebogo aliweka rekodi ya kitaifa kwa kukimbia kwa sekunde 9.88 na alikuwa na haya ya kusema baada ya mbio hizo.

Noah Lyles ashinda mbio za mita 100 huko Budapest katika mashindano ya riadha ya dunia
Noah Lyles wa Marekani akisherehekea baada ya kushinda huko BudapestPicha: Matthias Schrader/AP/picture alliance

"Naifurahia sana medali ya fedha na kwetu sisi, ni ufanisi wa ziada kwasababu lengo kuu lilikuwa kufika fainali tu, kwa hiyo kushinda medali ni jambo bora zaidi kwangu na kocha wangu," alisema Tebogo.

Ferdinand Omanyala wa Kenya ambaye ndiye bingwa wa Jumuiya ya Madola na bingwa wa Afrika pia, alimaliza katika nafasi ya saba.

Omanyala anasema hafahamu kilichotokea ila alihisi mwili wake hauendi kwa kasi aliyotaka. Bingwa mtetezi Fred Kerley wa Marekani hakufuzu fainali hiyo hivyo hakuweza kulitetea taji lake.

Chanzo: DPAE/APE/Reuters