1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Taiwan yasema China yafanya majaribio ya kivita

25 Septemba 2024

Wizara ya Ulinzi ya Taiwan imesema kuwa China imefanya mazoezi ya kurusha silaha kali za kivita na mazoezi mengine ya kijeshi karibu na fukwe zake.

https://p.dw.com/p/4l2za
Ndege ya kivita ya China kwenye anga ya Taiwan.
Ndege ya kivita ya China kwenye anga ya Taiwan.Picha: Taiwan Ministry Of National Defe/ZUMA Wire/picture alliance

Taarifa iliyotolewa siku ya Jumatano (Septemba 25) na wizara hiyo ilisema kuwa imezitambuwa ndege 23 za kivita zikifanya shughuli zake kuzunguka kisiwa hicho.

Taarifa hiyo inajiri wakati China yenyewe ikisema kuwa jeshi lake limefanikiwa kufanya majaribio ya makombora ya masafa marefu yanayoweza kuvuuka mabara kwenye Bahari ya Pasifiki.

Soma zaidi: China yaionya Ujerumani baada ya meli yake kupita Taiwan

Hata hivyo, taarifa ya wizara ya ulinzi ya China ilisema kwamba majaribio hayo hayakuelekezwa nchi wala shabaha yoyote na kwamba yalifanywa kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Harakati za kijeshi za China kwenye eneo hilo zimekuwa zikizusha wasiwasi kwamba huenda Beijing inakusudia kutumia nguvu za kijeshi kutwaa mamlaka kamili ya kisiwa cha Taiwan, ambacho inakitambuwa kuwa ni sehemu ya miliki yake.

Taiwan ilijitangazia uhuru na kujitenga na China Bara.