1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroTaiwan

Taiwan yaripoti harakati mpya za kijeshi za China

27 Aprili 2024

Taiwan imeripoti leo kuhusu harakati mpya za kijeshi za China karibu na kisiwa hicho kinachojitawala huku ndege 12 zikiwa zimevuka mpaka usio rasmi wa mlango wa bahari wa Taiwan.

https://p.dw.com/p/4fFbY
Meli ya kivita ya China huko Taiwan
Meli ya kivita ya jeshi la wanamaji la China ikiwa kwenye Bahari ya TaiwanPicha: Handout/Government Produced/AP Photo/picture alliance

Hayo yanaripotiwa siku moja baada ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani kumaliza ziara yake nchini China.

Wizara ya ulinzi ya Taiwan, imesema kuwa kuanzia leo asubuhi, ilikuwa imegundua ndege 22 za jeshi la China pamoja na ndege za kivita aina ya Su-30, ambazo 12 zilivuka mpaka huo usio rasmi kuingia Taiwan kupitia eneo la Kaskazini na Kati.

Soma pia:Taiwan, China zinaweza kutatua tofauti zao, asema rais wa zamani baada ya kukutana na Xi

Wizara ya ulinzi ya Taiwan, imesema ndege hizo zilihusika katika doria za pamoja za utayari wa mapigano pamoja na meli za kivita za China, na kuongeza kuwa ndege na meli za kisiwa hicho zilijibu ipasavyo.

Hata hivyo wizara hiyo haikutoa maelezo zaidi. Wizara ya ulinzi ya China haijazungumzia chochote kuhusu madai hayo.