1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hofu juu ya kuenea kwa homa ya nyani yaripotiwa Kongo

26 Juni 2024

Watafiti wametahadharisha juu ya kuenea kwa kirusi kipya cha homa ya nyani ambacho kinaripotiwa kuwa hatari na kinasambaa kwa kasi zaidi.

https://p.dw.com/p/4hXmk
Affenpocken
Picha: Isai Hernandez/imago images

Hivi karibuni, kirusi hicho kimeripotiwa kusababisha vifo vya watoto na kuharibu mimba za wanawake wajawazito nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Watafiti wameeleza wasiwasi wao kuwa kirusi hicho huenda kimesambaa katika nchi jirani.

Kongo yatangaza mripuko wa homa ya nyani

Mtafiti katika chuo kikuu cha Rwanda anayehusika na magonjwa ya mlipuko, John Claude Udahemuka, amesema mataifa yote yanapaswa kuwa macho kutokana na kirusi hicho cha homa ya nyani. 

Mlipuko wa ugonjwa wa homa ya nyani uliotokea mwaka 2022, ulisambaa katika zaidi ya nchi 110, huku ukiathiri zaidi wanaume wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.