1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Taarifa ya habari, saa 12:00 Asubuhi (Afrika Mashariki)

Daniel Gakuba
4 Januari 2021

https://p.dw.com/p/3nTqD

-Kanda ya sauti imepatikana ambamo Rais Donald Trump wa Marekani anasikika akimshinikiza kamishna wa uchaguzi katika jimbo la Georgia kutafuta kura za kumsaidia Trump kushinda jimbo hilo katika uchaguzi wa rais wa Novemba iliyopita.

-Bunge la Marekani limewachagua viongozi wake wapya, wiki mbili na nusu tu kabla ya rais mteule Joe Biden kuchukua madaraka rasmi.

-Waasi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wameushambulia mji wa Bangassou, siku moja kabla ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi wa rais ulioandamwa na ukosoaji.