1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sydney: Mtuhumiwa wa ugaidi afutiwa mashitaka

27 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBen

Maafisa nchini Australia wameyafuta mashitaka ya ugaidi dhidi ya daktari wa kihindi aliyekamatwa kuhusiana na jaribio lililoshindwa la kuripua bomu lililotengwa garini nchini Uingereza . Dr Mohammed Haneef mwenye umri wa miaka 27, alishitakiwa kwa kusaidia katika njama hiyo kwa kumpa jamaa yake anayeishi Uingereza kadi ya simu yake ya mkononi. Alikua gerezani tangu tarehe 3 mwezi huu, alipokamatwa akijaribu kuondoka Australia kuelekea India.

Waziri wa uhamiaji wa Australia amesema leo kwamba Haneef atabakia gerezani, hadi uamuzi utakapotolewa kuhusu suala la kuhamia kwake nchini humo.