1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sunak akutana na Macron mjini Paris

10 Machi 2023

Waziri Mkuu wa Uingereza, Rishi Sunak leo amekutana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron mjini Paris katika mkutano wa kilele kati ya nchi hizo mbili.

https://p.dw.com/p/4OWP7
Paris | Sunak bei Macron
Picha: Le Pictorium/Imago

Mkutano huo unalenga kuzungumzia mvutano wa miaka mingi kuhusu Brexit na mkataba mpya wa wahamiaji wanaotumia ujia wa bahari unaoitenganisha Uingereza na Ufaransa.

Sunak alipongeza uhusiano kati ya nchi hizo, kabla ya mkutano huo, ambako viongozi hao wanatarajia pia kuahidi msaada kwa Ukraine na usalama katika eneo la Asia-Pasifiki.  Macron alimkaribisha Sunak  katika Ikulu ya Ufaransa Elysee, baada ya kuwasili Paris kwa treni.

Huo ni mkutano wa kwanza kati ya Uingereza na Ufaransa kufanyika katika kipindi cha miaka mitano, baada ya Sunak kuwa waziri mkuu Oktoba, mwaka 2022.