Kenya yashutumiwa kuruhusu mazungumzo ya RSF
19 Februari 2025Hayo yanajiri baada ya Rais Ruto kuruhusu wanamgambo wa Sudan waliowekewa vikwazo kufanya mkutano jijini Nairobi ili kuzindua serikali mjini Khartoum.
Kwenye taarifa kwa vyombo vya Habari, Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imesema kuwa inasikitishwa na kupuuzwa kwa serikali ya Kenya kwa wajibu wake chini ya sheria za kimataifa, Mkataba wa Umoja wa Mataifa, Mkataba wa Umoja wa Afrika, na Mkataba wa Kuzuia na Kuadhibu Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari kwa kuandaa hafla yaZaidi ya watu 200 wauawa katika siku tatu za mashambulizi ya Sudan kusaini kile kinachoitwa makubaliano ya kisiasa kati ya wanamgambo wa kigaidi wa Janjaweed wanaohusika na vitendo vinavyoendelea vya mauaji ya kimbari nchini Sudan na watu na makundi yao yanayohusiana.
Soma pia:RSF yaishambulia kambi ya wakimbizi ya Zamzam
Taarifa hiyo imeongeza kusema kuwa, kwa kuanzisha serikali sambamba katika sehemu ya ardhi ya Sudan, kunachochea mgawanyiko wa mataifa ya Afrika, kunakiuka uhuru wao, na kuingilia masuala yao ya ndani.
Vikosi vya RSF, ambavyo ni moja ya makundi yanayopigana na yanayotuhumiwa kwa mauaji ya kimbari katika vita vya muda mrefu vya Sudan, vilikutana katika KICC siku ya Jumanne kupanga uzinduzi wa kile walichokiita, Serikali ya Amani na Umoja. Abdel Aziz Al Hillu ni mwenyekiti wa Jeshi la Ukombozi la Sudan, SLA.
"Tumeanza kutafuta amani na mazungumzo katika taifa geni, kwa hivyo ningependa kumshukuru Rais, serikali na wananchi wa kenya.”
Kenya yakanusha kukika makubaliano
Taarifa hiyo imesema kuwa hatua hiyo ya serikali ya Kenya si tu inakiuka misingi ya ujirani mwema bali pia inakiuka ahadi ambazo Kenya imefanya katika ngazi za juu zaidi kuhakikisha kuwa hakuna shughuli za uhasama dhidi ya Sudan zitakazofanyika katika ardhi yake.
Hata hivyo Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje nchini Kenya, Korir Sing'oei, amekanusha madai kwamba Kenya inaunga mkono kundi RFS na kuongeza kuwa inapendekeza suluhisho la mazungumzo katika mzozo huo.
Soma pia:UN yaomba msaada wa dola bilioni 6 kwa Sudan kwa mwaka huu wa 2025
Miongoni mwa wahudhuriaji wa hadhi ya juu kwenye hafla hiyo jijini Nairobi alikuwa Naibu Kamanda wa RSF, Abdulrahim Hamdan Dagalo, ambaye amewekewa vikwazo na Marekani.
Hamdan ni kaka yake kamanda wa RSF, Luteni Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, ambaye anapigana dhidi ya Jeshi la Sudan linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan.
Sudan sasa inataka jamii ya kimataifa kuingilia kati suala hilo ambalo huenda ukaibua uhasama kati ya mataifa hayo mawili.