1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Sudan na Iran zarejelea uhusiano wa kidiplomasia

10 Oktoba 2023

Sudan na Iran zimetangaza kupitia taarifa ya pamoja kurejeshwa kwa uhusiano wao wa kidiplomasia baada ya kusitishwa kwa takriban miaka saba

https://p.dw.com/p/4XKCC
Waziri wa mambo ya nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian
Waziri wa mambo ya nje wa Iran Hossein Amir-AbdollahianPicha: Maxim Shemetov/AP Photo/picture alliance

Katika taarifa iliyochapishwa mtandaoni, wizara ya mambo ya nje ya Sudan, imesema kuwa mataifa hayo mawili yamekubaliana kuchukuwa hatua zinazohitajika kufungua balozi zao katika nchi hizo hivi karibuni.

Iran na Sudan kuimarisha ushirikiano

Shirika la habari la serikali ya Iran, limeripoti kuwa pande hizo mbili zilikubaliana kuimarisha ushirikiano katika nyanja tofauti ambao unaweza kutimiza maslahi ya mataifa hayo mawili na kuhakikisha usalama na utulivu katika kanda hiyo.

Viongozi wa mataifa hayo mawili walikutana Baku

Waziri wa mambo ya nje wa Iran Hossein Amir-Abdollahian, na mwenzake wa Sudan, Ali al-Sadiq, walikutana mjini Baku nchini Azerbaijani mwezi Julai, huu ukiwa mkutano wa kwanza unaojulikana wa maafisa wakuu wa mataifa hayo mawili tangu mwaka 2016.