1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Stockholm:Mkutano wa kuzuia ukeketaji waendelea:

11 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CEEd
Mkutano wa kimataifa wa kuzuia zoezi la Wanawake kukeketwa barani Afrika na miongoni mwa familia za Wahamiaji nchini Sweden unaofanywa Stockholm leo umeingia siku yake ya pili. Wanaoshiriki mkutanoni wametoa mwito wa kushirikiana zaidi kwa lengo la kukomesha mila hizo. Maafisa wa serikali ya Sweden wamesema kuwa Wasichana na Wanawake wapatao millioni 130 ulimwenguni kote wamekeketwa wakati ambapo wengine millioni mbili hukeketwa kila mwaka. Maafisa hao wameongeza kusema kuwa jinsi Wahamiaji wa Kiafrika wanavyozidi kuwa wengi nchini Sweden ndivyo ambavyo tatizo hili limekuwa la kitaifa katika nchi za Scandinavia. Miongoni mwa wale wanaohudhuria mkutano huo ni Wajumbe kutoka nchi kumi za Kiafrika ambazo ukeketaji ni jambo la kawaida. Baadhi ya nchi hizo ni Tanzania, Kenya, Somalia, Eritrea, Ethiopia, Mali, Nigeria, Senegal na Misri. Mkutano wa Stockholm unahudhuriwa pia na Wajumbe wa Umoja wa Mataifa, Wabunge na mashirika ya kiutu.