1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Starmer aitisha mkutano wa dharura kujadili ghasia

5 Agosti 2024

Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, anatarajiwa kufanya mkutano wa dharura na wakuu wa polisi nchini humo baada ya siku kadhaa za maandamano ya vurugu ya kupinga uhamiaji.

https://p.dw.com/p/4j7Bx
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer.
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer.Picha: Ben Bauer/PA/dpa/picture alliance

Katika vurugu hizo, majengo na magari yameteketezwa kwa moto huku hoteli wanamolala wageni wanaotafuta hifadhi nchini Uingereza zikishambuliwa.

Wiki iliyopita, machafuko yalizuka katika sehemu mbalimbali nchini humo baada ya wasichana watatu kuuawa katika shambulio la kisu mjini Southport, kaskazini magharibi mwa Uingereza huku watu 420 wakikamatwa hadi sasa.

Soma zaidi: Waziri Mkuu Starmer aapa kuwawajibisha walioshiriki ghasia

Machafuko hayo yamechochewa na taarifa za uongo zilizosambazwa mitandaoni na makundi yanayopinga wahamiaji na Waislamu kwamba waliohusika na mauaji ya wasichana hao watatu ni Muislamu mwenye itikadi kali za kidini aliyewasili Uingereza hivi karibuni.

Polisi, hata hivyo, wamesema mshukiwa wa mauaji hayo ni mzaliwa wa Uingereza na hawalichukulii tukio hilo kama la kigaidi.