1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSomalia

Somalia yasema wapiganaji 49 wa al Shabaab wameuliwa

24 Novemba 2022

Serikali ya Somalia imesema wapiganaji 49 wa kundi la al Shabaab wameuliwa katika operesheni ya kijeshi kwenye eneo la Lower Shabelle.

https://p.dw.com/p/4JzRB
Somalia mehrere Tote bei Angriff auf Hotel Hayat in Mogadischu
Picha: Feisal Omar/REUTERS

Tukio hilo linafuatia kampeni inayoendelea kwa miezi kadhaa kwa lengo la kulidhibiti eneo linaloshikiliwa kwa muda mrefu na wapiganaji wa al Shabab.

Kundi hilo lenye mafungamano na kundi la kigaidi la al Qaeda linadhibiti maeneo mengi ya nchi ya Somalia na limedai kuhusika na mashambulio ya mabomu ya mwezi uliopita yaliyosababisha vifo vya takriban watu 120 katika mji mkuu wa Mogadishu.

Jeshi la Somalia lawaua wapiganaji 20 Al Shabaab

Waziri Mkuu Hamza Abdi Barre amesema katika taarifa yake kwamba vikosi vya serikali, vinavyoungwa mkono na wazee wa koo na wanajeshi wa Umoja wa Afrika, wamepata mafanikio katika vita dhidi ya al Shabaab katika miezi mitatu iliyopita.