Soko la mitumba "Flohmarkt"
29 Agosti 2013Matangazo
Leo tupo katika soko moja la hapa mjini Köln. Ni soko linaloitwa Flohmarkt ambapo wanaouza hapa si watu wanaofanya shughuli hiyo kama kazi yao rasmi bali ni watu wa kawaida tu wanaokusanya vitu nyumbani kwao, vitu ambavyo hawavihitaji tena. kwa kawaida vitu hivyo huuzwa kwa bei rahisi. Mara nyingi utakuta nguo, viatu, pochi, vitu vya nyumbani kama vikombe, sahani na hata vitu vingine vya zamani. Wakati mwingine utapata hata vitabu vya zamani ambavyo havipo tena madukani ila ukija katika soko kama hili unaweza kuvipata. Nikiangalia hapa naona watu wengi wamekuja na meza zao, wameleta bidhaa zao na wamezitandaza na wanajaribu kuzinadi na kuvutia wateja ili waje kununua vitu kwao.