1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Soka. Materazzi kuchunguzwa na FIFA.

14 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG7w

Shirikisho la kandanda duniani FIFA limeanzisha uchunguzi wa kinidhamu kuhusiana na jinsi alivyohusika mlinzi wa mabingwa wa dunia Itali, Marco Materazzi wakati wa fainali ya hivi karibuni dhidi ya Ufaransa.

Alipigwa kichwa na mchezaji nyota wa kiungo wa Ufanransa Zinedine Zidane ambaye alisema siku ya Jumatano kuwa Materazzi aliitukana mara kadha familia yake wakati wa mchezo huo. FIFA imewaita wachezaji wote katika kikao cha kusikiliza uchunguzi huo baadaye mwezi huu.