1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaKenya

Shule zafunguliwa Kenya baada ya janga la mafuriko

Saleh Mwanamilongo
13 Mei 2024

Zaidi ya asilimia 90 ya shule nchini Kenya zimefunguliwa leo, baada ya kufungwa kwa takribani wiki mbili kutokana na mafuriko yaliyosababisha vifo vya watu 270.

https://p.dw.com/p/4fo3Z
Kenya| Mafuriko
Mafuriko yaliyoyakumba maeneo mengi ya Kenya Aprili 2024, yalilazimisha kufungwa kwa shule kwa majuma kadhaa. Picha: Brian Ongoro/AFP/Getty Images

Kulingana na naibu msemaji wa serikali Mwanaisha Chidzuga, baadhi ya wanafunzi ambao shule zao zimeathirika sana, wataendelea na masomo katika shule zingine za karibu.

Awali, serikali nchini humo ilipanga kufungua shule tarehe 29 mwezi uliopita baada ya likizo ya wiki tatu, lakini ililazimika kuahirisha mara mbili kutokana na uharibifu wa barabara na shule.

Shule zipatazo 2,000 nchini humo, ziliathirika na mafuriko ikiwemo uharibifu huku baadhi ya familia zikikosa makazi.

Mafuriko makubwa yaliyochangiwa na mvua za masika zilizoambatana na hali ya hewa ya El Nino, yamesababisha watu takribani 300,000 kuondoshwa katika makazi yao na 75 hawajulikani walipo. Bado kuna wasiwasi kwamba idadi inaweza kuongezeka.