1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Shambulizi la Urusi laua watatu nchini Ukraine

21 Septemba 2024

Kamandi ya jeshi la anga la Ukraine limekadiria kwamba idadi jumla ya mashambulizi ilikuwa 25 huku makombora matano na droni 11 zilidunguliwa.

https://p.dw.com/p/4kvcC
Kyiv-Ukraine
Uharibifu wa jengo katika mji wa kiviwanda wa Kryvyi Rih kusini mwa Ukraine uliotokana na shambulio la Urusi.Picha: REUTERS

Takriban watu watatu, akiwemo mvulana wa miaka 12,wameuawa katika mashambulizi mapya ya makombora ya Urusi katika eneo la kusini la mji wa viwanda wa Ukraine wa Kryvyi Rih, mamlaka katika eneo hilo zimesema katika taarifa yake mapema hii leo.

Gavana wa mkoa wa Dnipropetrovski Serhiy Lyssak ameandika katika mtandao wa kijamii wa Telegram kwamba watu wengine watatu walijeruhiwa katika shambulio hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo na lililohusisha makombora ya chapa Iskander-M.

Soma zaidi. Mtoto wa Museveni asema hatowania urais 2026

Gavana huyo amechapisha pia picha mbalimbali zinazoonyesha nyumba zilizoathirika na shambulizi huku akiongeza kwamba juhudi za kuwatafuta walionusurika zinaendelea.

Mikoa kadhaa nchini Ukraine iliripoti pia mashambulizi ya anga ya Urusi usiku kucha.

Kamandi ya jeshi la anga la Ukraine limekadiria kwamba idadi jumla ya mashambulizi ilikuwa 25 huku makombora matano na droni 11 zilidunguliwa.