1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulizi la kisu lauwa mwanamke mzee wa miaka 70 Israel

4 Agosti 2024

Polisi wa Israel na madaktari wamesema mwanamke mwenye miaka 70 ameuawa na watu wengine watatu wamejeruhiwa katika shambulio la kisu kwenye kitongoji kimoja cha mji wa Tel Aviv.

https://p.dw.com/p/4j5dW
Mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za Israel huko Tel Aviv
Watu wanaonekana kwenye eneo lililowekewa kizuizi ambapo mripuko ulitokea huko Tel Aviv mnamo Julai 19, 2024.Picha: Gil Cohen-Magen/AFP/Getty Images

Kulingana na polisi, mshambuliaji huyo alikuwa mkazi wa Ukingo wa Magharibi, ikiashiria kuwa shambulio hilo la Jumapili hii lilitekelezwa na mpiganaji wa Kipalestina. Idara ya uokoaji ya Israel imesema watu wengine wawili, wamejeruhiwa katika mkasa huo huku mmoja wao akiwa na hali mbaya.

Msako mkali unaendelea katika eneo hilo. Mvutano umeongezeka katika ukanda huo tangu kufanyika kwa shambulizi la Hamas la Oktoba 7 mwaka jana huko Gaza.