1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Mtu mmoja auawa katika shambulizi la anga la Israel

14 Juni 2024

Mtu mmoja ameuawa katika shambulizi la anga lililofanywa na Israel kwenye nyumba moja kusini mwa Lebanon. Watu wengine zaidi ya saba wamejeruhiwa kwenye shambulizi hilo.

https://p.dw.com/p/4h3V9
Mashambulizi katika Ukanda wa Gaza
Israel imeendelea kushambulia Ukanda wa Gaza na shambulizi la leo limesababisha kifo cha mtu mmoja kusini mwa LebanonPicha: Bashar Taleb/AFP/Getty Images

Kulingana na vyanzo vya usalama vya Lebanon raia aliyeuwawa ni mwanamke na miongoni mwa waliojeruhiwa ni watoto.

Hata hivyo jeshi la Israel limesema linachunguza ripoti hiyo iliyotolewa na Shirika la Habari la Taifa la Lebanon.

Shambulizi la Israel limejiri baada ya Hezbollah inayoungwa mkono na Iran kudai kuhusika na mfululizo wa mashambulizi ya roketi na ndege zisizo na rubani kwenye vituo vya kijeshi vya Israel upande wa kaskazini.

Haya yanajiri huku wizara ya afya ya Gaza inayoendeshwa na Hamas imesema watu 37,266 wameuawa katika ukanda huo katika vita vilivyodumu kwa zaidi ya miezi minane kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas.