1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Shambulio la Urusi laua kichanga na kujeruhi watu Ukraine

6 Februari 2024

Mtoto wa miezi miwili ameuawa na watu watatu wengine wamejeruhiwa leo kufuatia shambulio la Urusi kaskazini mashariki mwa Ukraine.

https://p.dw.com/p/4c5dH
Ukraine| Urusi| Mapigano
Mapigano kati ya Urusi na Ukraine yamekuwa yakisababisha vifo na uharibifu mkubwa Picha: Ukrainian Emergency Service/AP Photo/picture alliance

Gavana wa eneo hilo Oleg Sinegubov ameeleza kuwa, hoteli ya ghorofa tatu imeharibiwa katika kijiji cha Zolochiv baada ya Urusi kufanya mashambulizi kadhaa ya makombora aina ya S-300.

Kijiji cha Zolochiv kiko takriban kilomita 20 kutoka mpaka wa Ukraine na Urusi.

Kulingana na gavana Sinegubov na taarifa ya idara ya polisi ya Ukraine, shambulio hilo limesababisha kifo cha mtoto wa miezi miwili na kuwajeruhi watu watatu akiwemo mama wa mtoto huyo.

Polisi imeongeza kuwa, majengo 30 pia yameharibiwa ikiwa ni pamoja na mikahawa, soko, maduka ya kuuza dawa na hoteli.

Mkoa wa kaskazini mashariki wa Kharkiv umekumbwa na mashambulizi ya makombora hivi karibuni tangu wanajeshi wa Ukraine walipochukua tena udhibiti wa sehemu kubwa ya eneo hilo.