1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulio la droni lazua moto kwenye ghala la mafuta Urusi

13 Julai 2024

Makombora ya Urusi katika mkoa wa Kherson wa Ukraine yamewaua watu wawili wakati nchi hizo mbili zikiendeleza mashambulizi ya droni kuanzia usiku wa kuamkia leo

https://p.dw.com/p/4iFus
Ukraine Kyiv
Moja ya jengo lililoharibiwa na shambulizi la Urusi huko Kyiv, UkrainePicha: Ori Aviram/Middle East Images/AFP/Getty Images

Makombora ya Urusi katika mkoa wa Kherson wa Ukraine yamewaua watu wawili wakati nchi hizo mbili zikiendelea kushambuliana kwa ya droni kuanzia usiku wa kuamkia leo.

Katika mkoa wa kusini-magharibi wa Rostov wa Urusi, ghala la mafuta huko liliteketezwa kwa moto kufuatia shambulio la droni za masafa marefu zinazotumiwa na wanajeshi wa Ukraine kuyashambulia maeneo ya maeneo ya mpakani mwa Urusi.

Soma zaidi. Zelensky akutana na waziri mkuu wa Ireland

Mbali na mashambulizi hayo ya droni, Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema imedungua droni zingine katika maeneo ya mikoa ya magharibi ya Kursk na Belgorod mapema hii leo.

Vadym Filashkin, Gavana wa mkoa wa Donieski nchini Ukraine ameripoti kwamba shambulizi la Urusi limesababisha vifo vya watu sita na kuwajeruhi wengine 22 katika eneo hilo la mashariki mwa nchi hiyo.