1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Afrika kuutumia mkutano wa mazingira kupata ufadhili zaidi

23 Agosti 2024

Nchi za Afrika zinakusudia kuutumia mkutano wa Umoja wa Mataifa juu ya tabia nchi ili kuweza kupata fedha zaidi kwa ajili ya kupambana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

https://p.dw.com/p/4jpbu
Kenya | Athari za mafuriko
Kenya ni moja ya nchi zilizoathiriwa na mvua kubwa. Msichana huyu amesimama juu ya gari lililofunikwa na udongo katika eneo lililoathiriwa a mafuriko katika kijiji cha Kamuchiri, karibu na Mai Mahiu, Aprili 29, 2024.Picha: LUIS TATO/AFP

Wajumbe wa Afrika wameandaa orodha ya mikakati watakayoiwasilisha kwenye mkutano wa matayarisho utakaofanyika nchini Ivory Coast mwezi ujao.

Nchi za Afrika mpaka sasa zinapata chini ya asilimia moja tu kwa ajili ya kukabaliana na madhara yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Kiwango hicho kinawakilisha dola bilioni 100, wakati bara la Afrika linahitaji vitega uchumi vyenye thamani ya dola trilioni 1.3 kwa ajili ya miradi ya tabia nchi.