1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Ufaransa: Serikali yanusurika kura za kutokuwa na imani nayo

21 Machi 2023

Bunge limeidhinisha jana mswada tata wa pensheni unaoongeza umri wa kustaafu nchini Ufaransa kutoka miaka 62 hadi 64.

https://p.dw.com/p/4OyFh
Themenpaket | Frankreich Proteste gegen Rentengesetz
Picha: GONZALO FUENTES/REUTERS

Hii ni baada ya wajumbe katika bunge la taifa kupinga miswada miwili ya kutokuwa na imani na serikali. Lakini mswada huo wa pensheni uliosukumwa na Rais Emmanuel Macron bila idhini ya wabunge bado unahitaji kupitiwa na Baraza la Katiba kabla ya kutiwa saini kuwa sheria.

Soma pia: Serikali ya Ufaransa yakabiliwa na kura ya kutokuwa na imani nayo

Baraza hilo lina mamlaka ya kukataa vifungu ndani ya miswada lakini kwa kawaida huwa linaiidhinisha. Mswada wa kwanza wa kutokuwa na imani, uliopendekezwa na kundi dogo la siasa za mrengo wa kati likiungwa mkono na wa mrengo wa kushoto, uliponea chupuchupu idhini ya wabunge, kwa kupata kura 278 kati ya 287 zinazohitajika ili kupitishwa.

Mswada wa pili, uliowasilishwa na chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha National Rally, ulipata tu kura 94 katika bunge hilo.