1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Scholz atembelea maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko

31 Desemba 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz ametembelea maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko kaskazini magharibi mwa taifa hilo, ambako mito imefurika.

https://p.dw.com/p/4akPv
Ujerumani Verden 2023 | Kansela Scholz atembelea eneo la mafuriko
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz anaitazama mto Weser unaofurika wakati alipotembelea eneo la mafuriko mnamo Desemba 31, 2023 huko Verden, Ujerumani.Picha: Alexander Koerner/Getty Images

Katika siku za karibuni, mamia ya watu wamekuwa wakihamishwa kutoka kwenye maeneo yaliyoathirika kaskazini na mashariki mwa Ujerumani, ikiwa ni hatua ya tahadhari.

Kansela Scholz aliwasili katika mji wa Verden, kwenye jimbo la Lower Saxony mapema leo ambako mitaro ya kando ya mito ilikuwa imefurika maji yanayokaribia kuvunja kingo zake katika baadhi ya maeneo ya jimbo hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari karibu na mto Aller, uliosababisha mafuriko katika maeneo ya Verden, Scholz aliwashukuru polisi, idara ya zimamoto, idara ya shirikisho inayoshughulikia misaada na vikosi vya jeshi kwa juhudi zao za pamoja.

Aidha, Kansela Scholz ameahidi serikali ya shirikisho kusaidia majimbo yaliyoathirika, na mamlaka ya maeneo katika kukabiliana na mzozo huo.