1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SEOUL:Korea ya kusini haitaki mazungumzo na Korea ya kikomunisti

7 Julai 2006
https://p.dw.com/p/CG9o

Korea ya kusini imekataa pendekezo la Korea ya Kaskazini juu ya nchi mbili hizo kufanya mazungumzo kwa lengo la kupunguza mvutano kwenye mpaka wao wa pamoja.

Serikali ya Korea ya kusini imeeleza kuwa huu si wakati mujarabu kwa mazungumzo hayo kufanyika. Korea ya kikomunisti ilipendekeza mazungumzo hayo yafanyike baina ya wajumbe wa kijeshi wa nchi hizo.

Korea ya kaskazini imetoa pendekezo hilo siku mbili baada ya kufanya jaribio la makombora ya masafa marefu, hatua ambayo imesababisha lawama kutoka kwa jumuiya ya kimataifa.

Wakati huo huo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linaendelea na mjadala juu ya mswada wa azimio juu ya kuiwekea vikwazo Korea ya kaskazini kwa sababu ya kufanya majaribo hayo.

Lakini nchi hiyo imesema itafanya majaribio zaidi.